Timu ya taifa ya Brazil imefanikiwa kuitandika Ecuador 3-0 kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi iliyofanyika jana usiku.

Mshambuliaji wa Barcelona,  Neymer junior alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake goli la kwanza kwa mkwaju wa penati  huku beki wa kushoto wa Ecuador, Walter Ayovi akajifunga goli la pili na goli la tatu likafungwa na Gabriel Jesus.

Brazil ilitawala mchezo huyo muda wote ambapo wapinzani wao walishindwa kuonesha cheche mbele ya wacheza samba hao baada ya kukubali goli 3-0 na kuifanya Brazil ijiongezee alama tatu muhimu kwenye harakati za kuelekea nchini Urusi mwaka 2018.

Neymar: Akiwatoka mabeki wa Ecuador wakati wa mechi ya kufuzu kombe la dunia ambapo Brazili alishinda 3-0.
Neymar Jr: Akiwatoka mabeki wa Ecuador wakati wa mechi ya kufuzu kombe la dunia ambapo Brazili alishinda 3-0.

Ushindi huo unakuja siku kadhaa baada ya Brazil kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki yaliomalizika hivi karibuni katika jijini la Rio nchini Brazil kwa kuifunga Ujerumani kwa mikwaju ya penati.

Kwa upande mwingine Argentina nao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Urugway bao hilo lifungwa na mshambuliaji Lionel Messi.

Pia Paraguay nao wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chile huku magoli ya Paraguay yakifungwa na Oscar Romero na beki Paulo da Silva huku bao pekee la Chile likifungwa na kiungo Arturo Vidal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *