Brazil jana imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ujerumani kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika jijini Berlin nchini Ujerumani.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa mataifa hayo mawili kukutana uwanjani tangu Ujerumani walipowaaibisha Brazil 7-1 katika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Jesus aliwaweka Brazil mbele kwa mpira wa kichwa dakika za mwishi mwisho kipindi cha kwanza, dakika ya 37.

Alikuwa amepoteza nafasi nyingine ya kufunga muda mfupi awali na kipindi cha pili alipoteza nafasi nyingine pia ambapo aliumpiga mpira nje kwa kichwa lango likiwa wazi baada ya Trapp kutokea kujaribu kuudaka mpira kona ilipopigwa.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Ujerumani ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia na walioorodheshwa nambari moja duniani kushindwa tangu walipolazwa na Ufaransa nusu fainali Euro 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *