Timu ya taifa ya Brazil imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya soka duniani.

Kwa mujibu wa viango vipya vilivyotolewa na Shirikisho la soka duniani (FIFA) Brazil imeendelea kukalia kiti hicho cha uongozi wa soka duniani.

Brazil imeendelea kushika nafasi hiyo kutokana na ubora wake aliouonesha kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia katika bara la Amerika ya Kusini na kupelekea kuwa timu ya kwanza duniani kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Argentina imeshika nafasi ya pili, nafasi ya tatu ni Ujerumani, nafasi ya Nne ni Chile, nafasi ya tano ni Colombia ,nafasi ya sita ni Ufaransa.

Nafasi ya saba imeshikwa na Ubeligiji, nafasi ya nane ni Ureno ,nafasi ya tisa ni Switzerland na nafasi ya kumi ni Hispania.

Kwa upande wa Afrika Misri bado ni vinara ikiwa katika nafasi ya 19 Ulimwenguni na orodha nyingine ya ubora Duniani itatoka tena Juni Mosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *