Timu ya Taifa ya Brazil imekuwa timu ya kwanza kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 baada ya kuifunga Paraguay 3-0.
Brazi jana walifanikiwa kushinda goli 3-0 dhidi ya Paraguay huku wapinzani wao wakaribu Argentina na Uruguay wakipoteza mechi zao.
Kutokana na matokeo hay Brazil hawaweza kumaliza chini ya nafasi nne katika msimamo wa mataifa ya Amerika Kusini ambapo mataifa ya kwanza manne ndiyo yanafuzu moja kwa moja.
Magoli ya Brazil kwenye dhidi ya Paraguay yalifungwa na mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar na mchezaji wa Real Madrid Marcelo.
Pia katika mechi hiyo Neymar alikosa mkwaju wa penalti na kufanya matokeo kuwa 3-0 kwenye mechi hiyo iliyofanyika nchini Brazil.