Mwanamuziki nyota wa Marekani, Shad Moss maarufu kama “Bow Wow” anatarajiwa kuungana na muimbaji mwenzake Christina Aguilera kwenye kipindi kipya cha TV kiitwacho ‘Tracks’ hivi karibuni.

Kipindi hicho kinatarajiwa kuanza kuonyeshwa kuanzia Septemba 1 mwaka huu na kitakuwa kinahusu watu tofauti kuweza kutaja majina ya nyimbo zinazochezwa kwa sekunde chache zaidi.

WEST HOLLYWOOD, CA - APRIL 23: Singer Christina Aguilera arrives at NBC's "The Voice" Season 8 red carpet event at Pacific Design Center on April 23, 2015 in West Hollywood, California. (Photo by Angela Weiss/Getty Images)
Christina Aguilera

Bow Wow anatarajiwa kuwa mtangazaji wa kipindi hiko huku Christina Aguilera akiwa mtayarishaji wa show hiyo.

Bow Bow ambaye kwasasa amejikita zaidi katika utangazaji alijizolea umaarufu mkubwa katika anga ya muziki nchini Marekani katika miaka ya 2000 baada ya kuachia nyimbo kama vile “Like You” akimshirikisha mwanamuziki, Ciara na “Let me hold you” aliyomshirikisha mwanamuziki Omarion.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *