Mwanamuziki wa Marekani wa nyimbo za hip hop, Shad Moss maarufu kwa jina la Bow Wow ametangaza kustaafu kuimba muziki atakapofikisha umri wa miaka 29, mwaka huu.

Bow Wow ametoa tangazo hilo kupitia mtandao wake wa Twitter.

Romeo

Mwaanamuziki huyo alianza kutoa albamu yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 13, mwaka 2000 na kupata umaarufu kupitia fani hiyo ya muziki nchini Marekani.

Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni “Like You” akimshirikisha mwanamuziki, Ciara na “Let me hold you” akimshirikisha mwanamuziki Omarion.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *