Bournemouth wamekamilisha usajiri wa winga wa klabu ya Liverpool, Jordon Ibe kwa mkataba wa miaka minne ambao umevunja rekodi ya klabu hiyo baada ya kuigharimu paundi milioni 15.

Winga huyo mwenye miaka 20 amecheza mechi 58 akiwa na Liverpool baada ya kujiunga nao akitokea klabu ya Waycombe Wanderers mwaka 2011.

Mchezaji huyo ameamua kuihama timu hiyo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kocha Jurgen Klopp ambapo ameanza mechi 12 tu za Ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *