Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imepinga taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano haitatumika tena baada ya Disemba 31 mwaka huu.

Mkurugenzi wa huduma za kibenki wa BoT, Marcian Kobello amesema kuwa noti kuwa noti ya shilingi mia tano itakuwepo kwenye mzunguko sambamba na sarafu ya shilingi mia tano hadi hapo noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.

Pia Kobello amewataka wananchi kuachana na taarifa hizo kwamba si za kweli kabisa kwani noti hizo bado zitatumika kama kawaida.

Serikali iliamua kureta sarafu ya shilingi mia tano baada ya noti ambayo ndiyo inazunguka zaidi kuchakaa mapema mikononi mwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *