Uchunguzi dhidi ya boss wa zamani wa kampuni ya magari ya Ujerumani ya VW, Martin Winterkorn huenda ukaanza hivi karibuni kuhusiana na udanganyifu uliokuwa ukifanyika wakati wa uongozi wake.

Mwendesha mashtaka wa Ujerumani amedai kuwa boss huyo huenda alikuwa anafahamu juu ya udanganyifu kuwa gari za kampuni hiyo zilikuwa zikitoa moshi wenye sumu.

Martin Winterkorn ambaye aliachia ngazi mwaka 2015 baada ya kampuni ya VW kukiri kutumia software kupunguza uchafuzi wa hewa katika gari zake zinazotumia dizeli.

Tangu wakati huo amekuwa akikanusha kufahamu endapo kulikuwa na ukiukwaji wowote wa taratibu hadi ilipofika mwezi Agosti mwaka 2015 muda mfupi baada ya bosi ya kampuni hiyo kutoa ripoti ya kugundua tatizo hilo.

Baada ya taarifa hiyo ya bodi ya VW, Martin Winterkorn akachukua hatua ya kuacha kazi mwezi Septemba.

Hata hivyo ofisi ya mwanasheria wa Ujerumani inahisi kuna mchezo wa makusudi ulikuwa unafanyika na hivyo wameamua kumchunguza boss huyo.

Tayari nyumba nyumba 20 zilizopo kwenye mji wa Braunschweig nchini Ujerumani zimeshafanyiwa uchunguzi zikihusishwa na kashfa hiyo.

Pamoja na nyumba hizo kuchunguzwa pia idadi ya washukiwa wa kashfa hiyo wameongezeka kutoka 21 hadi 37 akiwemo Winterkorn.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *