Beki wa Juventus, Leonardo Bonucci amesaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomuweka klabuni hapo mpaka msimu wa mwaka 2021.

Beki wa timu ya taifa ya Italiano alihusishwa kujiunga na aliyekuwa kocha wake wa Juventus Antonio Conte katika klabu ya Chelsea.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29 alijiunga na mabingwa hao Italiano akiokea klabu ya Bari mwaka 2010 ambapo hadi sasa amecheza mechi 291 katika klabu hiyo ya Juventus.

Toka ajiunge na Juventus ameshinda makombe matano ya ligi ya Italiano mfululizo, makombe matatu ya kombe la Italiano na amefanikiwa kucheza fainali ya kombe la dunai mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *