Aliyekuwa muigizaji nguli wa Bongo Movie, Marehemu Steven Kanumba leo amefikisha miaka mitano toka kifo chake kilipotokea mwaka 2012.

Kutokana na siku hiyo ya kumbukumbu ya muigizaji huyo, wasanii wenzake ambao alifanya nao kazi wamemfanyia dua na kutembelea kabuli lake lililopo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.

Kwa pande wa muigizaji Steve Nyerere amesema kuwa wasanii wa tasnia ya filamu wanapaswa kumuenzi kwa vitendo Steven Kanumba ambaye leo ametimiza miaka mitano tangu kifo chake.

Steve alisema hayo leo wakati alipoungana na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies kufanya ibada fupi ya kumuombea Kanumba kwa Mungu kutokana na matendo yake aliyowaachia kama kumbukumbu kwao. Ibada hiyo imefanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

Steve Nyerere amesema kuwa “Leo siyo siku nzuri kwetu kama wasanii, ni siku ya majonzi, tunaamini Kanumba yupo sehemu salama huko aliko, niombe wasanii wenzangu tuwe na ushirikiano katika kumuenzi, tusimuenzi kwa visirani, sisi kama ndugu tuliokutana hapa tushikamane na familia katika kumuenzi Kanumba,”.

Muigizaji huyo alifariki terehe na mwezi kama wa leo baada kusukumwa na kuanguka chini na msanii mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kupelekea kupoteza maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *