Waigizaji wa Bongo Movie wamefanya maandamano katika Mtaa wa Aggrey, Kariakoo ambapo ni sehemu maarufu kwa kuuza kazi za sanaa (CD za filamu mbalimbali) za ndani na nje ya nchi.

Wasanii hao wamefikia uamuzi huo ikiwa ni kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ya nchi ambazo wamedai kuwa zinaporomosha soko la filamu za ndani hivyo kusababisha kazi zao zisifanye vizuri sokoni.

Katika maandamano hayo wasanii wa Bongo Movie walisikika wakiimba.

Movie za kikorea, Kihindi kwisha” wengine wakiitikia “Kwisha kabisa”.

“Hatutaki movie za nje, hatutaki movie za nje”

“Bai bai, bai bai, bai bai….”

“Uzalendo, uzalendo, uzalendo…”

Hayo yalikuwa baadhi ya maneno waliyokuwa wakiimba kuweka msitizo kuwa kwa sasa kazi zao ndiyo zinatakiwa zipewe kipaumbele ili sanaa iwanufaishe wasanii wa Tanzania na siyo vinginevyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *