Bondia Mohamed Matumla amefanyiwa upasuaji wa kichwa kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kupigwa na Bondia Mfaume mfaume katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika katika ukumbi wa Ndani wa taifa jijini Dar es salaam.

Promota wa pambano hilo Jocktan Masai amaesithibitisha kuhusina na tukio hilo lililotokea katika pambano lilsilo la Ubingwa amesema Matumla alipatwa na mkasa huyo katika raundi ya saba ya pambano.

Bondia huyo ambaye ni mtoto wa nguli wa ndondi nhini Rashid Matumla alipigwa na kupoteza fahamu katika raundi ya saba ya pambano hilo baada ya kupigwa vibaya maeneo ya kichwani.

Baada ya kupoteza fahamu alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata bondia huyo.

Bondia huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospatali ya taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *