Polisi mkoani Morogoro inamshikilia bondia, Francis Cheka kwa kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 28 baada ya kukataa kupambana.

Cheka anakabiliwa na kosa la kukataa kupanda ulingoni desemba 25 dhidi ya bondia Abdalha Pazi (Dulla Mbabe) wa jijini Dar es Salaam.

Promota aliyeandaa pambano hilo, Kaiki Siraji amefungua kesi katika Kituo cha Polisi cha Kawe kwakuwa Cheka alimbadilikia dakika za mwisho wakati walikuwa na makubaliano kimkataba ulio kwa mujibu wa sheria za ngumi nchini.

Bondia Cheka atapelekwa leo ataletwa Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kesi hiyo katika kituo cha Kawe ambako kesi ilifunguliwa Desemba 25 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *