Bondia wa Uingereza, Anthony Joshua jana amempiga KO bondia Wladimir Klitschko wa Ukraine katika raundi ya 11 na kushinda ubingwa wa uzito wa juu.

Mashabiki wa ndondi walishuhudia pigano la kukata na shoka ambapo, Joshua alimwangusha Wladimir katika raundi ya tano, na kwa mara ya kwanza katika taaluma yake, Joshua akaangushwa katika raundi ya 6

Joshua alinusa ushindi, baada ya kupata upenyu na kurusha ngumi ya kushtukiza ya mtunguo, iliyompa nafasi ya kumwangusha wladamir kwa msururu wa ngumi.

Pigano hilo lililoshuhudiwa na zaidi ya watu 90,000 katika uwanja wa Wembley mjini London, lilisimamishwa katika raundi ya 11 baada ya Joshua kumzidi nguvu Wladimir na kumuangusha.

Uwanja wa Wembley ulijawa kelele na shangwe wakati mwamuzi alisema Wladamir amezidiwa kabisa.

Joshua ana umri wa miaka 27 tu lakini anaonekana ni miongoni mwa mabondia hatari katika uzito wa juu kwani hadi sasa amepigana mapambano 19 na kushinda yote, tena kwa Knock Out yaani ‘KO’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *