Mtangazaji maarufu nchini Afrika Kusini, Bonang Matheba ametangazwa kuwa mshereheshaji wa tuzo za mwaka huu za MTV MAMA akichukua nafasi ya mchekeshaji Trevor Noah aliyetangaza kutoshiriki.

Trevor ametangaza kujitoa kwenye nafasi hiyo ya kusherehesha kwenye tuzo hizo kama ilivyotangazwa mwanzo sababu ikiwa ni kuumwa hivyo dokta wake akimtaka apumzike hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa aliyoiweka kwenye mtandao wake wa Twitter.

Baada ya kutangazwa kuchukua nafasi ya Noah, Matheba kupitia mtandao wa Instagram ameandika anashukuru kupewa nafasi hiyo kwenye tuzo kubwa kama hizo.

Tuzo hizo zinafanyika Oktoba 22, 2016, kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini.

Future, Yemi Alade, Ycee, Alikiba, Cassper Nyovest, Diamond Platnumz, Babes Wodumo, Nasty C, Patoranking, Kwesta na Emtee wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tuzo hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *