Zaidi ya nyumba 250 zilizopo ndani ya mita 30 kutoka ilikopita reli ya kati jijini Dar es Salaam zimebomolewa kupisha ujenzi wa reli ya kisasa.

Bomoabomoa hiyo ilianza majira ya saa 10 alfajiri chini ya Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco) kupitia kampuni ya udalali ya Heputwa Investment.

Mmoja wa wananchi waliopitiwa na bomoa bomoa hiyo, Ramadhan Mbwana, mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, alisema Februari 5 mwaka jana, Rahco walifika eneo hilo wakiwa na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa na kuwataka wawepo kuhakikisha futi inavyopimwa hadi mwisho wa nyumba.

Mbwana amesema vipimo hivyo viligusa eneo dogo la banda (nyumba) lake na alipatiwa notisi ya siku 30 ili kuvuja jambo ambalo alilitekeleza.

Pia amesema eneo hilo lina leseni za makazi ambazo ziko hai na kuna ambao wana hati kamili walizozitoa ardhi, akiwamo jirani yake ambaye alizimia wakati wa bomoa bomoa hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *