Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund imesema kuwa mwanariadha wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt atashiriki mazoezi na klabu hiyo kwa siku chache.

Bolt amekuwa akisema kwamba angependa kucheza soka baada ya kustaafu katika riadha ambapo ndiyo kulipompa umaarufu.

Lakini wakimkaribisha maafisa wa klabu hiyo wamesema kuwa hakuna hakikisho kwamba mwanariadha huyo ataichezea klabu hiyo katika siku za usoni.

Japokuwa mwanariadha huyo atashiriki mazoezi na Borussia Dortmund lakini ni shabiki mkubwa wa Manchester United ya Uingereza.

Bolt ameshinda medali tatu za dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika katika jiji la Rio nchini Brazil.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *