Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt amesema kuwa anastaafu riadha moja kwa moja na hatoweza kurudi tena baada ya kustaafu.

Bolt ni mshindi wa dhahabu mara nane katika Olimpiki, amestaafu kutoka kwenye riadha baada ya kung’aa sana na kujizolea umaarufu si haba.

Bolt amesema kuwa “Inasikitisha kwamba inanilazimu kuondoka sasa,” alisema raia huyo wa Jamaica, ambaye alikimbia kuzunguka uwanja kuwaaga wachezaji uwanja wa michezo wa London Jumapili usiku wa kufungwa kwa mashindano hayo.

Bolt alishinda shaba mbio zake za mwisho za mita 100 kisha akaumia na kushindwa kumaliza mbio za kupokezana vijiti za 4x100m Jumamosi usiku.

Hii ina maana kwamba bingwa huyo wa dunia mara 19, ambaye Lord Coe alimfananisha na Muhammad Ali, aliondoka kwa njia isiyo ya kawaida – akisaidiwa kuondoka uwanjani na wenzake, akiwa hawezi kusimama vyema wima baada ya kuumia.

Mwisho amemaliza kwa kusema kuwa “Nimedhihirisha ustadi wangu, mwaka baada ya mwaka, katika kipindi changu chote nilichoshiriki mbio hizi. Nilikuwa nasema kwaheri kwa kila kitu. Nilikuwa karibu kulia. Nilikaribia sana, lakini machozi hayakutoka.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *