Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt ameaga mashindano ya riadha nchini Jamaica kwa kushinda mbio za mita 100 katika ardhi ya nyumbani Jamaica.

Bolt mwenye umri wa miaka 30 ataaga riadha wakati anastaafu mwezi Agosti baada ya mashindano ya World Championships mjini London baada ya kuanza kuwaaga mashabiki wakae huko Kingston Jamaica.

Bolt alikimbia kwa kasi ya sekunde 10.03 mbele ya mashabiki 30,000 waliocheza densi na kupeperusa bendera huku fataki zikirushwa.

Mwanariadha huyo mwenye rekodi ya mita 100 na 200 alibusu uwanja baada ya kumaliza mbio hizo.

Waziri mkuu wa Jamaica Andrew Holness na rais wa chama cha kimataifa cha riadha Sebastian Coe pia walihudhuria.

Bolt ameshinda mbio za mita 100, 200 na na dhahabu ya 4×100 katika mashindano matatu ya olimpiki yakiwemo Beijing 2008, London 2012 na Rio 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *