Mwanariadha wa mbio fupi wa Jamaica na bingwa wa kihistoria wa mbio za mita 100 Usain Bolt, amepokonywa medali yake ya Olimpiki za mwaka 2008.

Uamuzi wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) umefikiwa baada ya mkimbiaji mwenzake wan chi hiyo Nesta Carter kuthibitika kuwa alitumia dawa na kusisimua misuli kwenye mbio za kupokezana vijiti.

Nesta Carter anadaiwa kutumia dawa aina ya methylhexaneamine ambazo zimepigwa marufuku michezoni.

Uamuzi wa IOC umeikuta timu nzima ya Jamaica iliyoshiriki mbio za kupokezana vijiti kwenye mbio za mita 4×100 hivyo kumfanya Bolt kusaliwa na medali 8 za Olimpiki alizoshinda kwenye mashindano ya mwaka 2008, 2012 na 2016.

Kwenye mbio za mwaka 2008, Carter alikuwa mkimbiaji wa kwanza wa Jamaica ambapo timu hiyo iliweka rekodi ya dunia kabla ya kuivunja tena mwaka 2012 jijini London.

Nchi ya Trinidad and Tobago ndio wanaojiandaa kutangazwa kuwa washindi wa medali ya dhajhabu ya mashindano hayo huku Japan akitarajiwa kuchukua medali ya fedha na Brazil wakipata shaba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *