Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge amezindua Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji (NWIF) na kuitaka ifanye kazi kwa kasi, weledi na ubunifu mkubwa, la sivyo hataona shida kuivunja wakati wowote.

Lwenge aliizindua bodi hiyo jana, wizarani, Dar es Salaam na kusisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeelekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha mwananchi wa kawaida ananufaika na rasilimali za nchi, hivyo bodi hiyo isiposimamia hilo, ataivunja.

Amewataka wajumbe wa bodi hiyo Grace Mwakilufi, Sixbert Qamdiye na Jackson Mutazamba iliyoanzishwa kwa kifungu cha 44 (1) cha Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Namba 12 ya Mwaka 2009 ambayo itakayofanya kazi kwa miaka mitatu kuanzia jana, wafanyake kazi kwa ubunifu ili kuisaidia serikali kuondoa kero za maji nchini kwa kuitumia vyema dhana ya “Hapa Kazi Tu.”

Akinukuu malengo ya uboreshaji wa huduma ya maji vijijini na mijini, Lwenge aliitaka bodi hiyo ifikapo mwaka 2020, huduma hizo ziboreshwe kwa asilimia 85 vijijini kutoka asilimia 72 ya sasa na asilimia 95 mijini kutoka asilimia 86 ya sasa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *