Bodi ya Wadhamini ya chama cha Wananchi (CUF), kimewasilisha maombi mahakamani wakitaka Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya na Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma wazuiliwe kwa muda kujihusisha na masuala ya uongozi pamoja na kufanya mikutano yoyote ya chama.

Wabunge hao wameshtakiwa pamoja na wenzao sita ambao ni Thomas Malima, Omari Masoud, Abdula Kambaya, Salama Masoud, Zainab Mndolwa na Jaffar Mneke.

Maombi hayo yamewasilishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, chini ya hati ya dharura na yamepangwa kusikilizwa kesho mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.

Wakili wa waombaji Hashimu Mziray ameomba maombi hayo yasikikizwe upande mmoja kesho na mahakama ilikubali ombi hilo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *