Mwanamuziki nyota wa hip hop nchini Marekani, Bobby Brown siku ya jumamosi alifanya sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wake, Kristina Brown ambaye alipoteza maisha Julai 26, mwaka 2015.

Kristina Brown juzi alikuwa anatimiza miaka 24, hivyo baba yake aliamua kumfanyia sherehe kama sehemu ya kumkumbuka huku akiweka picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii za enzi za uhai wake.

Hata hivyo, msanii huyo aliweka picha nyingine za mke wake marehemu, Whitney Houston, ambaye alifariki dunia Februari 11, mwaka 2012 na kumwachia mtoto mmoja Kristina Brown.

Bobby Brown aliandika maneno yafuatayo kwenye mitandao ya kijamii “Kristina alikuwa kama malaika kwangu, siku kama ya leo, tungekuwa pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 24, lakini ametangulia mbele ya haki ninaamini ipo siku tutakuja kukutana,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *