Klabu ya Swansea City ya nchini Uingereza imemfukuza kocha wake Bob Bradley kutokana na matokeo mabovu inayoipata klabu hiyo mpaka kupelekea hatari ya kushuka daraja.

Siku ya jumatatu Sanswea wakiwa katika uwanja wa nyumbani Liberty Studium walipata kipigo cha mbwa mwizi baada ya kufangwa 4-1 na West Ham kwenye mechi ya ligi nchini Uingereza.

Swansea inashika nafasi ya 19 juu ya Hull City wakitofautiana magoli wote wakiwa na alama 12 baada ya kucheza mechi 18 hadi sasa ambapo katika mechi 11 alizoongoza kocha huyo ameambulia kupata alama saba pekee.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkis amesema kuwa wameamua kufanya maamuzi hayo nusu ya msimu kuisha ili kuisadia timu hiyo kuepuka hatari ya kushuka daraja kutokana na matokeo mabovu wanayoyapata.

Kocha huyo ametumia siku 85 katika klabu hiyo baada ya kujiunga na Swansea City mwezi Oktoba mwaka huu akitokea klabu ya Le Havre ya nchini Ufaransa na kuweka rekodi ya Mmarekani wa kwanza kufundisha timu ya ligi kuu nchini Uingereza.

Swansea kwasasa itaongozwa kwa muda na Alan Curtis pamoja na Paul Williams kabla ya kocha mpya kutangazwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *