Rais wa zamani wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, Sepp Blatter amewasilisha rufaa yake ya mwisho mahakamahi dhidi ya kesi inayomkabili ya kukiuka maadali ya mchezo huo.

Blatter amehudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama ya usuluhishi wa migogoro michezoni nchini Uswizi.

Blatter alifungiwa kutojihusisha na masuala ya mpira mwezi Disemba mwaka jana kwasababu aliidhinisha malipo ya zaidi ya dola milioni mbili kwa rais wa zamani wa UEFA, Michel Platini miaka mitano iliyopita.

Platini alishindwa kushawishi kuondolewa kwa adhabu dhidi yake ingawa ilipunguzwa kutoka miaka sita hadi miaka minne hivi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *