Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka duniani (Fifa) Sepp Blatter amemlaumu rais wa sasa Gianni Infantino kwa kutopokea simu zake.

Blatter mwenye umri wa miaka 80 anasema alikutana na Infantino kujadili masuala ambayo yanaweza kusuluhishwa kwenye shirikisho la Fifa.

Kifungo cha miaka sita aliyopewa Blatter kutojishugulisha na shughuli zozote za  mpira ilifutwa wiki hii baada ya kukatwa rufaa.

Blatter amesema Nimemuuliza, nimemtumia barua na nina namba yake na niliambiwa bado iko sahihi, hawezi kupokea simu, hawezi.

Blatter alitimuliwa Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kulipa pauni milioni 1.3 kwa aliyekua mkuu wa Uefa Michel Platini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *