Mwanamitindo wa Marekani, Blac Chyna na mpenzi wake Rob Kardashian ambaye ni mtangazaji wa TV wameachana na kupelekea Rob kufuta picha zote za mpenzi wake huyo kwenye ukurasa wake wa instagram ingawa Blac Chyna bado anaoneka kuutaka uhusiano huo.

Rob aliamua kuchukua uamuzi wa kumuacha mpenzi wake huyo baada ya kuona ujumbe mfupi kwenye simu yake  ambao haukujulikana ulikuwa ni ujumbe gani kwani mpaka sasa Rob hajaweka hadharani.

Mastaa hao wawili wamedumu kwenye uhusiano kwa muda wa miezi saba ambapo uhusiano wao ulianza Januari mwaka huu.

Mwanzo uhusiano wao ulikuwa ukikataliwa na wanafamilia wa Kardashian lakini wao waliendelea na mahusiano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *