Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amesema kuwa hajafurahishwa kuhusishwa kwenye ugomvi unaoendelea baina ya wasanii Godzilla na Wakazi.

Billnas amesema kuwa kitendo hicho cha kuhusishwa kwake kinaweza kumsababishia mashabiki wake kutomuelewa kabisa.

Mwanamuziki anayetamba na wimbo wake ‘Mazoea’ amesema hayo baada ya bifu ya wasanii hao kuzidi kushika kasi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii nchini.

Billnass ameongeza kwa kusema kuwa siyo kitu kizuri sana kwa sababu ukisema Godzilla ana-stress halafu Billnass ndiyo anamsababisha unahisi mashabiki wa Godzilla wakiniona mimi si watasema huyu ndiyo kikwazo cha msanii wetu asifike mahali, kumbe kila mtu anachangamoto zake.

Pamoja na hayo Bill aliendelea kufunguka kwa kusema haamini kama Godzilla atakuwa na mawazo ambayo yamempelekea kugombana na wasanii wenzake.

Mwisho amemaliza kwa kusema kuwa aamini kama Godzilla ana ‘stress’, kwasababu Godzilla ni kati ya watu waliofanya vizuri kwa mfululizo, ana matukio mengi, ana mizizi kwenye huu muziki na bado ana nafasi kubwa kwenye hii tasnia”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *