Mkali wa Hip Hop Bongo, Billnas amesema yupo kwenye mazungumzo ya kuhamia katika lebo kubwa ya muziki hapa nchini hivi karibuni ambapo bado hajaweka wazi ni lebo gani atajiunga nayo.

Billnas ambaye kwasasa yupo chini ya label yake ya ‘LFLG’, amesema kuwa kuna lebo nyingi zinamtaka kufanya naye kazi na yeye yupo tayari kufanya hivyo kwasababu muziki ni biashara.

Mkali huyo ameendelea kusema kwamba “Kusema kweli kuna mambo makubwa yanakuja, huwenda kazi yangu mpya ikaja nikiwa ndani ya label mpya”.

 Billnas ameongeza kwa kusema kusema kuwa kuuna lebo nyingi zimekuja na bado nipo kwenye mazungumzo, nadhani muda ukifika mtasikia tu,”.

Billnas alianza kufanya vizuri na wimbo ‘Raha’ aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka Kenya Naaziz kipindi hiko akiwa Rada Entertainment inayomilikiwa na TID lakini baadae alihama na kujiunga ‘LFLG’.

Mkali huyo kwasasa anatamba na nyimbo yake inayokwenda kwa Chafu Pozi ambayo inaendelea kufanya vizuri hadi sasa.

Nyimbo zilizompa chati mwanamuziki huyo ni Raha, Ligi ndogo pamoja na ya sasa Chafu Pozi ambayo video yake ameitolea nchini Afrika Kusini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *