Wasanii wawili wa hip hop nchini ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye muziki wa bongo Darasa pamoja na Billnas wamefunguka na kutoa shukrani kwa msanii Mwana FA baada ya msanii huyo kuwatambua na kusema kuwa anawakubali wasanii hao kama wasanii wanaofanya vyema kwa sasa kwenye muziki wa Hip hop.

Shukrani hizo zinakuja baada ya Mwana FA kusema kuwa Billnas pamoja na Darasa ni wanamuziki ambao wanafanya muziki ambao wao wametaka uwe hivyo na wamepatia kwani wameweza kuufanya muziki wao kutokana na vile wao walitaka kufanya.

Kutokana na kauli hiyo Billnas pamoja na Darasa walikuwa na maneno haya kwa Mwana FA.

Bill Nas amesema “Nafurahi kuona hujawahi kuacha kuni support toka enzi za Lyimo mpaka kuwa Nenga.

Kwa upande wa Darasa alisema siku zote watu ambao wapo pamoja na wapo real watapeana support hivyo anamshukuru sana Mwana FA kwa kuweza kumtambua na kuonesha anamkubali na kukubali kazi anazofanya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *