Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni mmiliki wa hoteli za kitalii nchini,Maleu Mrema anatarajiwa kuzikwa katika eneo la hoteli Yake ya kitalii ya Ngurdoto iliyoko nje kidogo ya jiji la Arusha Agosti 9 mwaka huu.
Mrema amefariki hivi karibuni akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini katika hospitali ya City garden iliyoko katika mji wa Johannesburg.
Msemaji wa familia Vincent Laswai amesema kwamba baada ya vikao mfululizo vya familia wameafikiana marehemu azikwe katika eneo la hoteli yake ya Ngurdoto
Awali taarifa zilienea kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ambako alikozaliwa lakini taarifa hizo zimekanushwa na msemaji hiyo wa familia.
Laswai amesema kwamba mwili wa marehemu unatarajia kuwasili Agosti 7 mwaka huu kutoka nchini Afrika Kusini ambapo utapokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Amesema kwamba baadhi ya wanafamilia,ndugu ,Jamaa Na marafiki watakwenda kuupokea mwili huo katika uwanja wa ndege ambapo familia imetoa usafiri maalum kwa wale watakaoshiriki.