Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce anatarajiwa kutangaza kikosi chake kwa mara ya kwanza baada ya kumalizika kwa mechi za ligi kuu nchini Uingereza siku ya jumapili Agosti 28 mwaka huu.

Mechi ya kwanza ya kocha huyo itakuwa dhidi ya Slovania ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi itakayofanyika Septemba 4 huku mechi ya pili ikiwa dhidi ya Malta katika uwanja wa Wembley mwezi Oktoba.

Kocha huyo amesema katika kikosi chake atakachokitangaza atamjumuisha golikipa wa Manchester City Joh Hart japokuwa hana nafasi kwenye kikosi cha Pep Gurdiola msimu huu.

Vile vile kocha huyo amemteua kocha msaidizi wa Leicester City, Crag Shakespeare kuwa kocha wa kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Uingereza pia akimteua Sammy Lee kuwa kocha msaidizi na Martyn Margetson kuwa kocha wa magolikipa.

Kocha huyo alichaguliwa kuwa kocha wa Timu ya taifa ya Uingereza ambapo amechukua nafasi ya Roy Hudgson aliyejiuzuru baada ya kufungwa dhidi ya Island kwenye mashindano ya EURO nchini Ufaransa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *