Mwanamuziki wa miondoko ya mduara nchini, Ally Tall ‘AT’ amemwandikia maneno ya dharau na lawama msanii mwenzake wa Bongo fleva, Peter Msechu kupitia ukurasa wake wa instagram.

Mkali huyo wa mduara nchini kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika kama ifuatavyo

“Mvuto Sifuri Bikaka @peter_msechu Nene km Lori Hivi kuongelea wembamba wangu unalipwa sitaki shobo km lakufanya huna jikate minyama yako ujichome mishkaki usi nitekenye mdomo ukataka niongee,”.

Vile vile ameandika “Tumbo Tumbo km Umeficha Kobe wewe nipotezee usilazimishe mimi niwe karibu na wewe sina shida ya kukuazima tumbo nende nalo harusini Mifulana km Turubali za Msimbani Babu kaa mbali na mimi kwani hivi na wewe ni msanii wanchi hii au Muuza kufia za Oliva Mtukuzi?”.

msechu

Pia mwishoni alimaliza kwa kuandika “Pyuuuuuuuuuuuuu ukiona nipo kimya ujue sihitaji varangati na mtu kiki zime adimika huna utakapopatia usinione Mwembamba ingia 18 uhadithie wenzio Mr Machupi ya kushonesha.”

Kutokana na maneno hayo aliyoandika AT kunaonekana kuna tofauti kubwa iliyopo kati ya wasanii hao wawili ambapo hadi sasa haijulikani chanzo cha tatizo hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *