Mwanamuziki wa Marekani, Justin Bieber na mpenzi wake Sofia Richie wadaiwa kuachana baada ya kutoonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu.

Chanzo cha karibu cha wawili hao kimesema kuwa Bieber na Sofia hawajaonekana pamoja tangu mara ya mwisho walipokuwa vacation nchini Mexico wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Sofia aliyetimiza miaka 18.

Wikiendi hii Sofia alihudhuria kwenye sherehe ya Magazine Party akiwa na marafiki zake ambapo hakuonekana kuwa na mpenzi wake ambaye mara nyingi huwa pamoja na kuhudhuruia sherehe wakiwa pamoja.

Justine Bieber na Sofia Richie Wawili walianza kuwa na mahusiano tangu mwezi Agosti, mwaka huu ambapo sasa wanadaiwa kumwagana.

Justine Bieber ameonekana kukumbwa na kashfa nyingi katika mahusiano ambapo mwezi uliopita aliingia kwenye bifu zito na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi Selena Gomez baada ya kushambuliana kwenye mitandao ya kijamii.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *