Staa wa muziki nchini Marekani, Justin Bieber amefuta akaunti yake ya mtandao wa instagram baada ya baadhi ya mashabiki wake kumtukana mpenzi wake mpya.
Staa huyo na mpenzi wake wa zamani, Selena Gomez walikuwa wakishtumiana katika mtandao huo wa picha na video.
Tatizo hilo lilianza baada ya Justin Bieber kuweka baadhi ya picha akiwa na mpenzi wake mpya Sofia Richie.
Baada ya kutukanwa matusi kutoka kwa mashabiki wake alionya kuibinfasisha akaunti yake iwapo vijana wanaomtusi hawatasita kumtusi.
Bieber aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram “Iwapo nyinyi ni mashabiki wa ukweli msingewachukia watu ninaowapenda?”.
Inaonekana Bieber alifuta akaunti yake ya Istagram kwasababu ukifungua unapata maneno yanayokwambia ”samahani mtandao huu hautumiki”.
Selena Gomez aliandika komenti yake chini ya picha hiyo aliyoiweka Bieber akisema iwapo hutaki kushambuliwa acha kuweka picha ya mrembo wako.
Mara baada ya komenti hiyo ya Selena Gomez, Justin Bieber alijibu huku akidai katika ujumbe uliomaanisha kwamba msanii huyo alimtumia ili kupata umaarufu.