Refa Bibiana Steinhaus amekuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha mechi ya Ligi ya Kuu ya Ujerumani, Bundesliga baada yake kuchezesha mechi kati ya Hertha Berlin na Werder Bremen Jumapili ambapo ilimalizika kwa sare ya 1-1.

Matthew Leckie alifungua ukurasa wa mabao kwa kufungia Hertha, lakini Thomas Delaney akasawazisha kipindi cha pili.

Steinhaus, 38 aliteuliwa kuwa mwamuzi wa ligi kuu ya Ujerumani mwezi Mei baada ya kusimamia mechi za ligi ya daraja la pili kwa miaka sita.

Agosti, mwamuzi huyo ambaye ni afisa wa polisi alisimamia mechi ya mkono wa kwanza kati ya Bayern Munich na Chemnitzer katika michuano ya Kombe la Ujerumani.

Aidha, alisimamia fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya upande wa kina dada msimu uliopita.

Jumamosi, Lorraine Watson aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mwamuzi katika soka ya wanaume nchini Scotland baada ya kusimamia mechi ambapo Edinburgh City waliwashinda Berwick Rangers 1-0 katika Ligi ya Daraja la Pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *