Biashara za silaha za jadi zapigwa marufuku Dar

0
476

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku uuzwaji holela wa silaha za jadi kama vile mapanga, mishale, pinde na manati maeneo ya barabarani.

Katazo hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro baada ya wahalifu kutumia silaha za jadi kama mapanga kufanya uhalifu.

Kamanda Sirro amesema kuwa “Sasa ni Marufuku kwa mtu yeyote au kikundi chochote kuuza mapanga, kuuza manati, kuuza pinde hizi na mishale barabararani hapa mjini. Watu wote tunajua biashara ya mapanga huwezi kuifanya barabarani kama huna leseni, lakini pia kwasababu ni silaha tumeshawahi kuona madhara ya mapanga, unaweza kuuza mapanga kwa nia nzuri barabarani mwenzako anagombana na mwingine au kuna ugomvi kati ya mtu na mtu wanakuja wanakunyanga’nya lile panga wanaleta madhara’.

Kama Sirro ameongeza kwa kusema “Siku za nyuma iliwahi kutokea kwahiyo kuna watu wamekamatwa na mapanga tutawapeleka mahakamani kwa makosa yao. Kwahiyo napenda kutamka suala la uuzaji wa mapanga barabarani ni marufuku, suala la uuzaji wa mapanga pia ni marufuku kama nilivyoonyesha,suala la kuuza mishale na pinde barabarani ni marufuku,”.

 

 

LEAVE A REPLY