Staa wa muziki nchini Marekani, Beyonce ameongoza kwenye vipengele vya tuzo za MTV Music Awards 2016 baada ya kutajwa kwenye vipengele 11 vya tuzo hizo kupitia albamu yake mpya inayofanya vizuri ‘Lemonade’.

Baadhi ya vipengele alivyotajwa staa huyo ni Video bora ya mwaka, msanii bora wa kike na nyimbo bora ya kushirikiana huku staa mwingine wa muziki, Adele akifuatia baada ya kutajwa kwenye vipengele nane vya tuzo hizo.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Agosti 28 mwaka huu kwenye ukumbi wa New York’s Madison Square Garden nchini Marekani.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *