Mwanamuziki nyota nchini Marekani, Beyonce amelazimika kuahirisha tamasha lake la New Jersey linalojulikana kwa jina la ‘World Tour’ baada ya madaktari wake kumshauri kupumzisha sauti yake.

Beyonce ambaye amesheherekea siku yake ya kuzaliwa siku ya Jumapili ambapo amefikisha umri wa miaka 35, ametoa taarifa inayosema kwamba tamasha hilo halitafanyika tarehe 7 mwezi Septemba.

Lakini mwanamuziki huyo ataendelea na tamasha lingine katika miji ya Los Angeles, Houston, New Orleans na Atlanta kama ilivyopangwa.

Ziara hiyo ambayo inalenga kuuza albamu yake mpya inayoitwa ‘Lemonade’ ilianza mjini Miami mnamo tarehe 27 mwezi Aprili mwaka huu.

Tamasha hilo lilitarajiwa kukamilika katika mji wa Nashvile mnamo tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka huu lakini sasa inaonekana kwamba New Jersey itaanda tamasha lake la mwisho na mwanaumuziki huyo.

Beyonce ni mwanamuziki aliyejizolea umaarufu mkuwa kwa mashabuki wake dunia kote kwa kutoa nyimbo zinazokonga nyoyo za watu ambapo kwasasa ameanda tamasha hilo ili kuitangaza albamu yake mpya ya ‘Lemonade’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *