Mwanamuziki nyota wa Marekani, Beyonce alitawala tuzo za muziki za MTV zilizofanyika mjini New York hapo jana baada ya kupata jumla ya tuzo saba.

Beyonce alijishindia tuzo kubwa katika tamasha hilo baada ya kupata tuzo ya video ya mwaka kwa nyimbo yake ‘Formation’ ambayo inaelezea ubaguzi wa rangi, utumiaji wa nguvu kupitia kiasi unaofanywa na maafisa wa polisi pamoja na kimbunga Katrina.

Drake na Rihanna: Rapa Drake akimkabidhidi tuzo ya heshima mwanamuziki Rihanna kwenye tuzo za MTV hapo jana.
Drake na Rihanna: Rapa Drake akimkabidhidi tuzo ya heshima mwanamuziki Rihanna kwenye tuzo za MTV hapo jana.

Mwanamuziki huyo aliwasili katika sherehe hizo za utoaji wa tuzo na mama zao wanaume wanne Wamarekani weusi ambao vifo vyao vilizua hisia kali nchini Marekani.

Kwa upande mwingine mwanamuziki, Rihanna alitunukiwa tuzo ya mchango wake katika usanii kufikia sasa akiwa na umri wa miaka 28 pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *