Makundi mawili ambayo yalifuzu kushiriki hatua ya robo fainali katika shindano la Dance100% mwaka huu yameondolewa kushiriki katika shindano hilo kutokana na utovu wa nidhamu na kukiuka kanuni za shindano hilo.

Makundi yaliyotolewa ni Best Boys pamoja na P.O.D ambayo yote yalitakiwa yashiriki robo fainali ya Jumamosi tarehe 13 Agost viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Bw. Kurwijira Maregesi amesema katika mashindano yoyote duniani nidhamu ni kitu muhimu sana ambacho kinaweza kumfanya mshindanaji kufika mbali katika kufanikiwa kwenye maisha na shindano.

Maregesi ameongeza kuwa lengo la makundi hayo kuitwa ni kuweza kusaini mikataba ambapo mtu mmoja hawezi kusaini mkataba wa kundi zima hivyo makundi ambayo wametuma mtu mmoja watalazimika kupisha shindano na kuacha wenye nia kuendelea.

100

Jaji wa shindano hilo Super Nyamwela amewataka washiriki wote kuheshimu muda hasa katika kipindi hiki ambacho makundi hayo yanakutana na majaji kwa ajili ya kuweza kufundishwa namna ya kutawala jukwaa, kuchagua nyimbo, pamoja na kwenda na muda.

Makundi ambayo yatashiriki Dance100% Jumamosi katika mchuano wa robo fainali Jumamosi Agusti 13 ni B.B.K Crew Boys , Mazebe Powder , D.D.I Crew, The Quest Crew, The Hero’s Crew , Clevers Boys, Mafia Crew ,T.W.C Crew , Makorokocho Crew ,Ikulu Vegas Crew ,Wazawa Crew ,J Combat Crew.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *