Bernie Ecclestone aondolewa kuongoza mashindano ya Formula One

0
145

Mkurugenzi wa Formula One, Bernie Ecclestone ameondolewa kwenye nafasi hiyo baada ya Shirika la habari la Liberty la Marekani kukamilisha mkataba wake wa dola bilioni 8 ya kuumiliki mchezo huo.

Ecclestone mwenye umri wa 86 amesimamia mashindano hayo kwa zaidi ya miaka 40, ameteuliwa kama mwenyekiti mstaafu na atafanya kazi ya mshauri katika bodi hiyo.

Chase Carey, atahudumu katika nafasi ya Ecclestone ya mtendaji mkuu na kuongezea katika majukumu ya kuwa mwenyekiti

Liberty pia imemnunua meneja wa zamani wa magari ya Mercedes, Ross Brawn kwa mashindano ya F1.

Mkurugenzi wa ufundi wa zamani wa Ferrari ambaye alikuwa akifanya kazi kwa niaba ya mshauri wa Liberty ameteuliwa kuongoza kazi za ufundi katika kampuni ya mashindano ya F1.

Liberty ilianza kutaka kumiliki mashindano hayo ya magari ya langalanga mwezi Septemba lakini mwezi huu wamekamilisha masharti mawili ya kisheria yaliokuwa yamesalia.

Mpango huo ulikamilika siku ya Jumatatu na shirika la habari la Liberty linatarajiwa kubadilisha jina lake na kutumia jina la kundi la Formula 1.

LEAVE A REPLY