Benjamin Samweli Sitta amethibitishwa kuwa meya wa Kinondoni na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Mahakama hiyo imetupilia mbali upande wa pili wa Ukawa waliofungua kesi ya kupinga ushindi wa meya huyo wakidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki.

Ukawa walifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga ushindi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta huku walalamikaji wakiwa ni Mustapha Muro (aliyekuwa mgombea Meya Manispaa ya Kinondoni) na Jumanne Amir Mbunju (aliyekuwa mgombea Naibu Meya wa Manispaa hiyo) wote wakiwakilisha na Wakili wa CHADEMA, John Malya.

Kesi iliyofunguliwa dhidi ya Afisa Utawala wa Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samweli Sita (aliyetangazwa kuwa Meya) na Manyama Mangaru (aliyetangazwa kuwa Naibu Meya).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *