Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetngaza kipeperusha bendera nusu mlingoti kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinj.

Katibu mkuu ametoa maelekezo hayo kwa watendaji nchi nzima kupeperusha bendera nusu mlingoti kufuatia kifo cha gwiji huyo wa siasa.

Mashinji ametoa maelekezo hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam na kusema bendera zinapaswa kupeperushwa nusu mlingoti hadi mwili wa kiongozi huyo utakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Ndesamuburo amefariki dunia leo ghafla katika hospitali ya KCMC mjini Moshi alipokuwa anapatiwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *