Staa wa Bongo fleva, Ben Pol amesema kuwa baada ya kusikilizwa wimbo wa Darassa ‘Muziki’ wakati haujakamilika kwa mara ya kwanza aliwaza mambo mawili katika akili yake.

Ben Pol amesema kuwa mambo mawili aliyokuwa anawaza juu ya wimbo huo ni kuwa wimbo huo ulikuwa unahitaji mwimbaji pili aliona wimbo utakuwa wimbo bora hivyo anahitaji kupata lifti kwenye wimbo huo.

Mkali huyo amesema ilibidi amshawishi Darassa kwa kumwambia kuna sauti anataka kuiweka kwenye wimbo huo ili msanii yoyote akayekuja kuimba apite kwenye njia hizo.

Kwa upande mwingine Ben Pol amesema ameamua saizi kufanya kazi na watu ambao wanaweza kusimamia kazi zao na si wale ambao wanafanya kazi harafu wanaziweka ndani au hawazipi nguvu kazi hizo.

Ben Pol ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva kutokana na nyimbo zake kubamba mashabiki kutokana ubora wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *