Staa wa Bongo fleva, Benard Paul “Ben Pol” amesema kazi ya muziki imemsaidia mambo mengi sana katika maisha na kumwezesha kuiongoza familila yake kupitia kazi yake hiyo.

Ben Pol amesema kwasasa anawasomesha wadogo zake wawili na anawahudumia kila kitu kwa sababu wazazi wake wameshakuwa watu wazima na ufanisi kidogo umepungua kwa hiyo yeye ndiyo anawajibika kuhudumia familia.

Staa huyo kwasasa anatamba na wimbo wake “Moyo Mashine” ambao unafanya vizuri katika vituo vya Radio na TV mbali mbali nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *