Staa wa muziki wa RnB hapa nchini, Ben Pol amesema anatarajia kuachia remix ya wimbo wake ‘Moyo Mashine’ akiwa na mwanamuziki wa Nigeria, Chidinma ambapo maandalizi ya kazi hiyo imeshaanza.

Ben Pol amesema kwamba nyimbo hiyo pia itakuwa kwenye albamu yake mpya inayotarajia kutoka hivi karibuni.

Ben Pol ameongeza kwa kusema kwamba “Ngoma ambayo inakuja ni Moyo Mashine remix ambayo nimefanya na Chidnma kutoka Nigeria,” huku akiongeza. “Nilimsikilizisha nyimbo nyingi lakini aliupenda huo, nikaona sawa,.

Chidinma
Chidinma

Staa huyo pia amesema kuna nyimbo nyingine tena amefanya na mwanamuziki huyo na muda wake ukifika atauzungumzia huo wimbo.

Nyimbo zote zitakuwa katika album yake mpya ambayo integemea kutoka baada ya mwezi Disemba mwaka huu.

Ben Pol kwasasa anatamba na wimbo wake huo wa Moyo mashine ambao unaonekana kupokelewa vizuri na mashabiki wake baada ya kupata airtime sana kwenye media mbali mbali hapa nchini.

Ben Pol mwenyewe aliwahi kukiri kwamba wimbo huo ndiyo wimbo uliompa mafanikio makubwa kuliko nyimbo zake alizowahi kuzifanya baada ya kupigwa katika media za nje ya nchi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *