Wanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol, Baraka the Prince na Jux wamechanga Sh 800,000 kwa ajili ya kumsaidia msanii mwenzao, Jet Man, anayehitaji fedha kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa maradhi yanayomsumbua yanayomsababishia asiweze kutembea.

Ben Pol alifafanua kwamba, baada ya onyesho lao la Love, Melody and Lights, katika fedha walizoingiza walitoa Sh 500,000 na pia wasanii hao walinunua biti iliyotengenezwa na Jet Man kwa kila mmoja kutoa Sh 100,000 kila mmoja, zikawa Sh 800,000 wakampelekea msanii huyo ili zimsaidie.

Pia amesema “Katika fedha tulizoingiza tumetoa Sh 500,000 na pia tumeongeza kila mmoja Sh 100,000, imefika Sh 800,000 tumempa rafiki yetu na msanii mwenzetu kwa mapenzi yetu ili zimsaidie katika baadhi ya mahitaji yake,’’.

Ben Pol aliongeza kwamba, licha ya kusaidia kiasi hicho pia wasanii hao wakishirikiana na mchekeshaji Mc Pilipili wameandaa tamasha mkoani Dodoma ambalo pia watatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kumchangia msanii huyo mwenye uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya kufanyiwa tiba ya matatizo yanayomsumbua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *