Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ben Pol amefunguka na kusema kuwa anawashangaa watu ambao wameonesha kutopendezwa na wimbo wa Darassa ‘Muziki’ alioshirikishwa.

Kauli hiyo ya Ben Pol inakuja baada ya baadhi ya watu kuuponda wimbo huo huku wakisema si hip hop halisi kama zilivyo nyimbo zake nyuma.

Ben Pol alitumia mitandao yake ya jamii kuonesha kuwa hata ukifanya jambo kubwa na zuri ambalo linaweza kuwafurahisha watu wengi zaidi lakini wapo watu ambao watatokea na kukukatisha tamaa, kukuvunja moyo hivyo siku zote usivunjike moyo na maneno ya watu bali inatakiwa usimamie kile unachokiamini kwani ni vigumu sana kumfurahisha kila mtu katika dunia hii.

Kupitia akanti zake za mitandao ya kijamii Darassa amesema kuwa “Pamoja na kuvunja rekodi na pia mafanikio ambayo wimbo huu ‘Muziki’ umeleta na unaendelea kuleta, Eti kuna watu buku mbili hawakuuelewa, hapo ndiyo utaamini kwamba haiwezekani kuwafurahisha watu wote duniani, lazima atatokea/Watatokea vichwa ngumu kadhaa tu ambao hawatakuelewa unachofanya, focus, Stick to your plans, Move forward, Conquer” aliandika Ben Pol.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *